Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amefanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi
Fionnuala Gilsenan na kumueleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika
kuiamrisha sekta za maendeleo huku akiwataka waekezaji wa nchi hiyo
kuja kuekeza Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimkaribisha Balozi wa Ireland Nchini
Tanzania Fionnuala Gilsenan,mara baada ya kuwasili Ikulu Mjini Zanzibar
kwa ajili ya kusalimiana na Rais jana.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar, Dk. Shein
alimueleza Balozi Gilsenan kuwa Zanzibar inawakaribisha waekezaji kutoka
Ireland kuja kuenkeza katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta utalii.
Alimueleza balozi huyo kuwa Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika
sekta ya utalii na ndo maana juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa
na serikali anayoiongoza katika kuiimarisha sekta hiyo muhimu katika
kuchangia pato la taifa.
Kwa upande wa sekta ya kilimo Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekusudia kuiamrisha Mapinduzi ya Kilimo
kwa kutekeleza Sera na programu mbali mbali za kilimo.
Alimueleza kuwa lengo kuu la kuchukua hatua hiyo ni kuhakikisha wananchi
wa Zanzibar pamoja na taifa kwa jumla wanakuwa na uhakika wa chakula
wakati wote.
Aidha, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo hatua zinazochukuliwa na
serikali anayoiongoza katika kuimarisha sekta ya uvuvi ikiwa ni pamoja
na kuhakikisha uvuvi wa bahari kuu unatekelezwa kwa ufanisi mkubwa
kutokana na tija yake kwa wavuvi na taifa kwa ujumla.
Comments