Watu wanane wamekufa baada ya
nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la
Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la Kerio pia limekumbwa na
mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia
jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miili ya watu wanane
imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.Source BBC.
Comments