Mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais
Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam
jana
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C wa kwanza kushoto ni Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Msanii
wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C, jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais
Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika
jijini Dar-Es-Salaam chini ya uangalizi maalum.
Ray C
amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve ambaye pia
amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao umesaidia kurudisha hali
ya kawaida ya Ray C.
Rais
amempongeza Ray C kwa kukubali hali
yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo
chini ya uangalizi maalum.
Rais
amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona kabisa
na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika shughuli zake za
kujitafutia kipato na maisha.
Kwa
vile Ray C bado yuko katika
matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi atakapokuwa tayari kabisa
kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo tunaomba jamii impe ushirikiano huo na
kuheshimu taratibu zake za matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
Imetolewa
na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012

Comments