MIKUTANO ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba Mpya Visiwani
Zanzibar, imeingia dosari baada kuzuka ghasia na baadhi ya watu
kujeruhiwa kwa kuchomwa visu.
Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji warioba
Vurugu hizo ambazo chanzo chake ni siasa, zilitokana na wafuasi wa
baadhi ya vyama vya siasa, kuvamia mikutano iliyokuwa ikifanyika Unguja
na kusababisha hofu za kiusalama.
Baadhi ya maeneo ambayo wanasiasa hao walivamia mikutano ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na kusababisha ivunjike ni Shehia za Magomeni na
Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi.Hii ni mara ya kwanza ghasia kuzuka
katika mikutano ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya visiwani humo.
Tukio la kuchomana visu, lilitokea katika Shehia ya Mpendae baada ya
vurugu zilizosababishwa na vijana kuvamia mkutano uliokuwa ufanyike jana
mchana.
Vijana hao walianzisha ghasia hizo baada ya kutaka kuvunja utaratibu
uliokuwa umewekwa. Walitaka wakae mbele ya wengine waliokuwa
wametangulia katika mkutano huo.
Hatua hiyo ilipingwa na kuibua ghasia ziliozababisha watu kadhaa kujeruhiwa kwa visu.
Tukio jingine lililovuruga mkutano huo ni lile lililotokea katika Shehia
ya Magomeni, Jumatatu wiki hii baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya
makundi mawili yenye misimamo tofauti juu ya mfumo wa Muungano; kuna
wanaopinga na wanaoukubali.
Comments