Chama tawala nchini Afrika
Kusini kinajiandaa kwa mpambano wa uongozi wa chama ambao utaamua ikiwa
utaendeleza kile ambacho wengi wanatafsiri kama ukosefu wa kuondokana na
madhambi ya enzi ya ubaguzi wa rangi.
Au ikiwa itakuwa fursa ya kuondokana na historia
ya nchi na kuipa nchi hiyo ambayo ina uchumi mkubwa zaidi barani
Afrika, mustakabali mwema
Hapa kinyan'anyiro huenda kikawa
kikali kwa Rais Jacob zuma. Anatarajiwa kugombea muhula mwingine kama
kiongozi wa chama katika eneo la Mangaung, ambako chama cha ANC
kilizinduliwa karne moja iliyopita.ANC ikiwa na wingi wa wafuasi, yeyote
atayeshinda uongozi wa chama, bila shaka atashinda katika uchaguzi wa
urais utakaofanyika baadaye mwaka 2014.
Mwaka 2007, rais Zuma alisaidiwa kushinda
uchaguzi wa urais katika kongamano kama hili linalotarajiwa mjini
Polokwane, wakati alipomshinda aliyekuwa rais Thabo Mbeki.
Tangu chama cha ANC kuanza kupokea uteuzi wa
wagombea tarehe mosi Oktoba, wale wanaomuunga mkono Zuma kuongoza kwa
muhula wa pili, wanaonekana kuwa wengi ikilinganishwa na wale
wanaomuunga mkono naibu wa Zuma, Kgalema Motlanthe - ambaye ndiye
mgombea mwingine pekee.
Mafanikio ya Rais Zuma katika muhula wake wa
kwanza kama rais, yameonekana kuathirika kutokana na mauaji ya Marikana
ambako wachimba migodi 34 waliokuwa wanagoma waliuawa na polisi.Ilikuwa
wakati wa mgogoro kuhusu mishahara ya wachimba migodi hao katika mgodi
wa lonmin. Wakosoaji wake wanasema mtindo wa uongozi wa Zuma ambao ni wa
kujivuta, unachochea kudorora kwa uchumi pamoja na kukidhoofisha chama
cha ANC.
Kashfa nyingine ambayo inamkuba Zuma ambaye
wakati mwingine anajulikana kama Msholozi, ni madai ya kutumia vibaya
mali ya umma kukarabti nyumba yake kijiji kwao Nkandla.
Mdhibiti wa mali ya umma anachunguza ikiwa idara
ya serikali inafadhili ukarabati huo, wakati huu ambapo wachimba migodi
wanalipwa pesa kidogo sana.
Bwana zuma amekana kukiuka sheria akisema kuwa aliomba mkopo wa kufanya ukarabati huo.
Kashfa nyingine inayomzonga Zuma ni ile ya ufisadi. Kuna madai kuwa chini ya utawala wake , ufisadi umekita mizizi na kwamba familia yake inanufaika na mapendeleo kwa kupata mikataba ya kibiashara kwa sababu ya kutoka kwa familia ya uhusiano wao.
Kashfa nyingine inayomzonga Zuma ni ile ya ufisadi. Kuna madai kuwa chini ya utawala wake , ufisadi umekita mizizi na kwamba familia yake inanufaika na mapendeleo kwa kupata mikataba ya kibiashara kwa sababu ya kutoka kwa familia ya uhusiano wao.
Kikulacho ki nguoni mwako.
Mwandani wake ambaye sasa ni hasimu wake wa
kisiasa,bwana Mbeki alivunja kimya chake cha miaka minne alipoanza
kumshambulia Zuma kwa uongozi akisema kuwa ana wasiwasi kuwa Afrika
Kusini inakosa mwelekeo na kwamba wananchi wanakubali kuongozwa kwa njia
isiyo faa na ambayo baadaye itasababisha mzozo mkubwa.
Bwana Mbeki alisema "kwanza sielewi ambako nchi
hii inaelekea. Na sijui hatua ambazo naweza kuchukua kukabiliana na kitu
ambacho kinatishia nchi hii hasa nchi kukosa mwelekeo wa uongozi"
Changamoto kubwa kwa zuma hatioki kwa upinzani bali kwa chama chake.
Bwana Motlanthe, 63, ni mwanasiasa mwenye
kusifika kwa kuwa alikuwa mfungwa wa zamani wa kisiasa, lakini haonekani
kama anataka sana kuwania urais. Alihudumu kama rais wa nchi hiyo kwa
miezi sita baada ya aliyekuwa rais Thabo Mbeki kuondoka mamlakani.
Akilinganishwa na Zuma bwana Motlanthe hana sifa
kama za Zuma, yeye ni mtu ambaye hapendi kujionyesha kwa umma sana. Ni
msiri na mtulivu sana
Ameteuliwa kuwania urais na jimbo lenye utajiri mkubwa zaidi Afrika Kusini la Gauteng wakati majimbo sita kati ya tisa yanamuunga mkono bwana Zuma.
Anasema ana wakati mgumu kutafakari ikiwa atamenyana na Zuma kuwania urais.
Kgalema Motlanthe
Bwana Motlanthe anaungwa mkono na Julius Malema,
ingawa amepuuza uungwaji huo akisema vijana wa ANC hawana kura nyingi
katika kongamano la chama. Bwana Motlanthe hataki kutaifishwa kwa migodi
ya Afrika Kusini kinyume na anavyotaka Bwana Malema.
Ikiwa atagombea urais dhidi ya Zuma, huenda
akapatia chama cha ANC uhai , lakini akishindwa basi ndio itakuwa mwisho
wa maisha yake katika chama cha ANC Kwa nini bwana Zuma angali
anapendwa na wengi?
Mwisho wa fungate
Zuma anapendwa na wengi, na chini ya uongozi
wake, juhudi dhidi ya virusi vya HIV zinasemekana kuzaa matunda Pia nchi
yake iko chini ya muungano wa nchi zinazokuwa kwa kasi zaidi pamoja na
hayo mwenyekiti mpya wa muungano wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye
ni mke wa zamani wa Zuma, alichaguliwa kama mwenyekiti mpya wa Muungano
wa Afrika.
Wengi katika ANC wanaamini kuwa ikiwa Zuma ataongoza nchi kwa muhula mwingine, itakuwa nduio mwanzi wa mwisho wa chama cha ANC.Source http:www.bbc.co.uk
Comments