Bingwa wa uzito mara tano Floyd Mayweather amepokonywa mkanda wa WBO alioshinda kutoka kwa Manny Pacquaio mwezi Mei.
Mkazi huyo wa Las Vegas, Nevada, 38, alishindwa kuilipa WBO dola 200,000 ada ya kikwazo ambayo mwisho ilikuwa Julai 3.
Mayweather amekuwa akiwa na haki na taji hilo mpaka sasa, anasema
alipanga kufanya hivyo kufuatia ushindi wake wa alama dhidi ya Pacquaio.
Mmarekani mwezie Timothy Bradley ndiye atakayeushikilia mkanda huo,
Baada ya Mayweather kuishinda Pacquaio, alishatangaza kuwa ataachia
mataji yake yote ili kuwapa mabondia wadogo nafasi ya kushinda mikanda.
“Kamati ya Dunia ya Ubingwa wa WBO inaruhusiwa bila mbadala wowote
kuacha kumtambua Bw Floyd Mayweather Jr kama bingwa wa dunia wa WBO
welterweight na aachie taji lake,” ilisema taarifa hiyo kwenye
wboboxing.com.
Mayweather, ambaye bado anashikilia mikanda wa WBA na WBC, amepewa hadi Julai 20 kukata rufaa ya uamuzi huo.
Anatarajiwa kupanda tena ulingoni jijini Las Vegas Septemba 12, japokuwa bado hajataja mpinzani wake.
Comments