Uwanja wa Millennium mjini Cardiff nchini Wales utakuwa mwenyeji wa
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2017, UEFA imethibitisha.
Kamati kuu ya shirikisho linaoongoza soka barani Ulaya lilikubaliana
mjini Prague kwa ajili ya mkutano ambapo walijadili masuala tofauti,
ikiwemo kuteua eneo kwa ajili ya mashindano miaka miwili ijayo.
Cardiff imeelezwa kuwa wawaniaji wa mbele wa fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya 2017 na Uwanja wa Millenium ulithibitishwa kuwa mwenyeji
na katibu mkuu wa UEFA Gianni Infantino siku ya Jumanne.
Comments