Tume ya
Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kuongeza siku nne zaidi za uandikishaji wa
wapigakura kwa kutumia teknolojia ya BVR baada ya idadi kubwa ya wakazi
wa Dar es Salaam kuitikia wito wa zoezi hilo.
Awali
zoezi hilo lilikuwa likamilike leo, Julai 31, lakini sasa litaendelea
hadi Agosti 4, mwaka huu ili kukabiliana na idadi kubwa ya watu
waliojitokeza kujiandikisha.
Kwa
mujibu wa chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia shughuli zote za
uchaguzi nchini, hadi jana, zaidi ya wakazi 1,000,000 walikuwa
wamekwishaandikishwa jijini Dar es Salaam.
Ikizingatia
matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Nec inatarajia
kuandikisha jumla ya wakazi zaidi ya 2.8 milioni wa jiji hilo lenye
idadi kubwa ya watu nchini Tanzania.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Nec, Jaji Damian Lubuva, hadi sasa jumla ya
zaidi ya watu 18 milioni wamekwishajiandikisha wakati tume ilitarajia
kuandikisha watu kati ya 22 milioni na 23 milioni.
Comments