Wakati klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa ikizidi kusisitiza kuwa uhamisho wa mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria kwa asilimia kubwa umekamilika, kocha wa Manchester United Louis van Gaal amezungumza kitu cha kushangaza kidogo kuhusiana na Di Maria.
Di Maria alishindwa kuripoti July 25 San Jose kujiunga na timu na
kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Ligi Kuu… Baada ya mchezo wa International Champions Cup kati ya Man Uninted dhidi ya PSG kumalizika kwa Man United kufungwa kwa goli 2-0, Van Gaal akiwa kwenye press Conference alijibu hafahamu nyota huyo alipo.
Licha ya kocha wa PSG Laurent Blanc kuthibitisha kuwa mazungumzo
kuhusiana na uhamisho wa Di Maria yamekaribia kufikia ukingoni ingawa
Man Utd inataka pound milioni 28 ili imuachie nyota huyo.
‘Manchester United na Paris Saint Germain ni vilabu viwili vikubwa na
makubaliano yanaweza kuwa magumu lakini tunakaribia kufikia
muafaka’.Alisema Laurent Blanc
Di Maria alihamia Manchester United mwaka 2014 akitokea katika klabu
ya Real Madrid ya Hispania kwa dau la uhamisho pound milioni 59.7 kwa
mkataba wa miaka mitano kiasi ambacho kilileweka rekodi ya
uhamisho Uingereza.
Comments