Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limemtangaza rasmi Waziri wa
Ujenzi ambaye pia ni Mgombea Urais wa kwa Tiketi ya CCM John Pombe
Magufuli kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kagame katika
mchezo utakao wakutanisha wenyeji Yanga na Gor Mahia ya Kenya mtanange
utakao pigwa Tarehe 18 mwezi huu.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Afisa
habari wa TFF Baraka Kaziguto amesema kuwa magufuli atakuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi huo akiongozana na viongozi wengine wa serikali.Inatoka kwa mdau
Comments