Wabunge
wawili waliohama CCM hivi karibuni, James Lembeli na Ester Bulaya
wamepitishwa katika kura za maoni kuwania ubunge kupitia chama chao
kipya.
Wakati
Lembeli akipitishwa kwa kura za kishindo kuwania ubunge katika Jimbo la
Kahama Mjini, Bulaya alishinda katika nafasi ya viti maalumu baada ya
kushindwa katika kinyang’anyiro cha Jimbo la Bunda Mjini.
Wanasiasa hao sasa wanasubiri uteuzi wa Kamati Kuu ya Chadema utakaofanyika Agosti 5 na 6.
Ushindi wa Lembeli
Katika
uchaguzi huo wa juzi, mbunge huyo wa zamani wa Kahama aliwabwaga wenzake
13 aliogombea nao akipata kura 168 kati ya 262 zilizopigwa, akifuatiwa
na John Katibu aliyepata kura 45, Peter Shita (17) na Emmanuel Madoshi
aliyepata kura 10.(P.T)
Wengine
ni Muta Nyerere (4), Felician Maige (4), Zacharia Obadia (3), Tadeo
Mwati (2), Arnold Mtajwaka (2), Prosper Denga (2), Deusdedit Madinda
(1), Reuben Macheyeki (1). Victor Mbwana na Richard Makingi waliambulia
patupu. Katika uchaguzi wa viti maalumu, Winfrida Mwinula alishinda kwa
kura 34 akifuatiwa na Salome Makamba aliyepata kura 30.
Bulaya
Kama
isingekuwa ni kura za maoni za viti maalumu zilizomfuta machozi, Bulaya
alikuwa tayari ametupwa nje baada ya kuanguka katika Jimbo la Bunda
Mjini.
Bulaya
aliyekuwa miongoni mwa makada saba wa chama hicho waliokuwa wanawania
kuliwakilisha jimbo hilo, alipata kura 37 kati ya 182 zilizopigwa akiwa
nyuma ya Pius Masururi aliyeibuka mshindi kwa kura 65 na Magembe Makoye
aliyepata kura 40.
Baadaye
katika mkutano wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), uliofanyika
baadaye usiku, Bulaya alipata kura 71 kati ya 110 zilizopigwa na
kuwabwaga Godliver Masamaki aliyepata kura 31, Joyce Sokombi (4), Minza
Shani (3), Dk Jane Nyamsenda (1) na Alice Wandya aliyeambulia patupu.
Awali,
Bulaya alikwaa kisiki baada ya jina lake kuwa miongoni mwa waliokatwa na
kamati ya utendaji inayosimamia majimbo hayo wakidaiwa ni wageni katika
chama; wapenda fujo na matabaka, akiwa pamoja na Chacha Nyamhanga,
Sulemani Daudi lakini walirudishwa kundini baada ya kikao cha viongozi
na watiania.
Katika
Jimbo la Bunda Vijijini, Sulemani Daudi aliibuka mshindi kwa kura 84
kati ya 127 zilizopigwana kuwashinda John Masenza aliyepata kura 14, Dk
Lucas Webiro (11), Frank Mongateko (8), Edgar Chibura (5) na Mathias
Bandio aliyepata kura moja.
Comments