Manchester United imemaliza vibaya ziara ya Marekani kwa kupokea kichapo kutoka kwa Paris Saint-Germain.
Mshambuaji machachari Zlatan Ibrahimovic na Blaise Matuidi walipeleka kilio hiko kwa Manchester United kwa kuinyuka 2-0.
Mechi hiyo iliyochezwa Chicago ilikuwa ya mwisho na Man U wanajiandaa
kuambana na Tottenham katika ufunguzi wa Ligi Kuu msimu 2015-16 Agosti
8, 2015.Wachambuzi wa soka wamedai kuwa mlinda mlango David de Gea hakuwa katika ubora wake katika mtanange huo.
Comments