TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
15 Julai 2015
CUF NA UKAWA
Waheshimiwa waandishi wa Habari
Chama cha wananchi CUF tukiwa sehemu ya UKAWA tunaendelea na vikao
vya kuafikiana na maamuzi kwa hoja mbalimbali zinazohusu uimarishaji wa
malengo ya uanzishwaji wa UKAWA.
Katika kikao cha UKAWA kilichofanyika tarehe 14 Julai 2015 Collesium Hotel Dar es Salaam, CUF hatukuweza kushiriki kikao hicho.
Katika kikao cha UKAWA kilichofanyika tarehe 14 Julai 2015 Collesium Hotel Dar es Salaam, CUF hatukuweza kushiriki kikao hicho.
Sababu za kutoshiriki kwetu katika kikao hicho, kumetokana na sababu
za kikatiba za ndani ya CUF kwa kuwa katika maamuzi yote yanayohusu
masuala mazito ya kinchi kama haya,tuna desturi ya kukaa na kujadiliana
kama chama kwanza katika kuafikiana na jambo lolote lile muhimu kwa
maslahi ya taifa kama vyama vingine vinavyofanya.
Baada ya kikao cha UKAWA cha 11/07/2015 CUF tume kuwa na vikao
vinavyohusisha viongozi wakuu wa chama yaani Mwenyekiti,Naibu Katibu
Mkuu na wakurugenzi na jana tumeendelea na kikao.
Na ndio maana katika kikao cha UKAWA Mwenyekiti Prof.Lipumba na sisi viongozi wa kuu hatukuweza kuhudhuria.
Kutohudhuria kwa kikao cha tarehe 14 Julai 2015, hakuna mahusiano
yoyote na uvumi kwamba CUF imesusia au kujitoa katika UKAWA kama baadhi
ya mitandao ya kijamii au vyombo vya habari vilivyoripoti pamoja na
maneno ya chini kwa chini yanayoendelea kwa wananchi, bali ni kutokana
na baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la taifa kutoka mikoani na
wanachama wetu maeneo mengi ya nchi kuutaka uongozi wa Chama kusitisha
kwa muda kuhitimisha maamuzi ya kumpata mgombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupeperusha bendera ya UKAWA mpaka kuwepo kwa
ridhaa ya Chombo hicho cha kikatiba.
Aidha Chama kinatambua kwamba hivi sasa tumebakiwa na muda mfupi
kabla ya kuingia katika mchakato rasmi wa kuchukua fomu za serikali
kuomba kuteuliwa kuwania uongozi, hivyo Chama kimeitisha kikao cha
Baraza Kuu la Uongozi la taifa hapo tarehe 25 Julai 2015 ilikupata
Baraka ya chombo cha maamuzi kama ambavyo wenzetu washirika wa UKAWA
wamekwishapitia hatua hizi katika vyama vyao.
Watanzania watambue kwamba Nchi inapitia katika kipindi kigumu sana,
ongezeko la majimbo 26 ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya
Uchaguzi,kwa kipindi cha chini ya siku 45 kabla ya kuanza kampeni ni
changamoto ambazo UKAWA tunapaswa kuyafanyia kazi ili kuona namna gani
tunajipanga kwa mazingira haya.
CUF tuanaamini kwamba kwa maridhiano ya pamoja ndani ya vyama vyetu
na ndani ya UKAWA tutajenga UKAWA imara na hatimaye kuwa na mgombea
mmoja wa Urais,Wabungena madiwani wa UKAWA na hivyo kuiangusha CCM
kwenye uchaguzi wa Oktoba 25.
HAKI SAWA KWA WOTE
Magdalena Sakaya
Naibu Katibu Mkuu, Bara.
Magdalena Sakaya
Naibu Katibu Mkuu, Bara.
Comments