Mamia ya wanafunzi wadhurika baada ya kula pipi zilizoharibika nchini Ufilipino
Mamia ya wanafunzi wameipotiwa kufikishwa hospitalini baada ya kula pipi zinazodaiwa kuharibika siku ya Ijumaa nchini Ufilipino.
Mkuu wa polisi wa mkoa wa Surigao Del Sur, alitoa maelezo kwa waandishi wa habari na kusema kwamba pipi zilizotengezwa mjini Davao zimedhuru watu 370 wengi wao wakiwa ni wanafunzi.
Takwimu hizo zilitolewa kulingana na vyanzo vya hospitali za wilaya ya Madrid, Marihatag na Lianga.
Polisi wameamrishwa kufanya msako na kuwakamata wachuuzi wanaouza pipi hizo zinazodaiwa madhara kutokana na kuharibika.
Hadi kufikia sasa, wachuuzi wanane ikiwa ni pamoja
na watano waliokamatwa mjini Cagwait, wawili Tandag na mmoja Tagbiat,
wametiwa mbaroni na kufikishwa kituoni kwa ajili ya uchunguzi.
Pipi hizo zinazouzwa kwa bei ya chini mno zinaarifiwa kusababisha ulegevu na kutapika.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments