Chelsea wamezindua jezi mpya za ugenini kwa msimu wa Ligi Kuu 2015-16
zikiwa na wadhamini Yokohama Tyres, na zitaonekana kwenye mechi za
kujiandaa na msimu dhidi ya Barcelona wiki ijayo.
Kwa sasa Chelsea wako ziarani nchini Mareakani na mabingwa hao
watapambana na mabingwa wa Hispania jijini Washington Julai 28, wakati
nyota wao watakapovaa jezi nyeupe zikiwa na mistari myekundu na ya bluu.
Chelsea walizindua jezi za nyumbani mapema wiki iliyopita.
Comments