Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM Rais Jakaya Kikwete amezindua rasmi jengo jipya la chama chake mjini Dodoma.
Akizindua jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua watu mpaka elfu tatu kwa
wakati mmoja Rais Kikwete amesema jengo hilo halitatumika na CCM pekee
bali litakuwa pia ni kitega uchumi kwa chama hicho.
Ameeleza kuwa CCM inavitega uchumi vingi na hivyo ni vyema viongozi
wa chama hicho wakaona haja ya kuviendeleza badala ya kuviacha kama
vilivyo hivi bila kuingiza fiada yeyote.
Ukumbi huo unatarajiwa kutumika mara ya kwanza siku ya jumamosi
tarehe 11 Julai, 2015 katika mkutano mkuu wa chama hicho utakao toa jina
la mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Comments