Rapa anaye wakilisha Young Money Nicki Minaj amefunguka yake yaliyomkwaza kwa kutumia akaunti yake ya twitter.
Minaj, amewauliza swali waandaji wa tuzo za MTV kwa upande wa nchi ya
Marekani , ni kwa nini hawajaitaja video yake alioishirikiana na
Beyonce “ Feeling Myself “ kuingia kwenye kipengele cha video bora ya
mwaka ?.
Licha ya kushukuru kutajwa kwake kwenye vipengele vitatu ambavyo ni
Best Female Video, Best Hip Hop Video “Anaconda”, na Best Collaboration
“Jessie J, Ariana Grande, Nicki Minaj – “Bang Bang” “ , lakini Nicki
Minaj bado alihoji uwepo au kutajwa kwa video ya Feeling Myself.
Nick Minaj aliandika “Hey guys @MTV thank you for my nominations. Did
Feeling Myself miss the deadline or…? akimaanisha kwamba je video ya
Feeling Myself ilichelewa kutoka au ?.
Tuzo hizo za MTV, za huko Marekani zinatarajiwa kutolewa siku ya
jumapili ya augost 30 katika jiji la Los Angeles huku Miley Cyrus,
akitarajiwa kuwa host wa onyesho jilo.
Comments