Chelsea wamezindua jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2015/16 wakiwa na
wadhamini Yokohama Tyres, huku Diego Costa akionekana kiongozi wakati wa
kampeni za uzinduzi huo.
Jezi za mabingwa hao zimekuja na kauli mbiu: “Kama sio blue, itakuwa
blue,” kama adidas na Chelsea wakitegema wachezaji wenye malengo ya
kutawala soka la Uingereza na Ulaya.
Jezi hiyo itavaliwa wakati wa ziara za kujiandaa na msimu mpya nchini
Marekani, kwenye mechi dhidi ya New York Red Bulls, Barcelona na PSG,
huku wakibainisha katika tukio soka la mchangani mjini Harlem Julai 21.
Comments