Skip to main content

Mchakamchaka umeanza Arusha, wagombea Ubunge CCM wamwaga sera

unnamed (1)
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha, Justine Nyari, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kujinadi nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi katika kata mpya ya Sinoni jijini Arusha
unnamed
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha, Mustafa Panju akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Sinoni kuhusu nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi ambapo amewataka wanaccm kudumisha mshikamano kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi ili kupatikane ushindi wa kishindo.
unnamed (2)
Emmanuel Ole Njoro ambaye ni Mgombea nafasi ya Ubunge jimbo la Arusha mjini akijinadi katika kata ya Sinoni.
unnamed (3)
Thomas Munis mgombea Ubunge akijinadi kwa wananchi wa Sinoni.
unnamed (4)
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akitoa maelekezo kwa wananchi  namna ya kuwasikiliza wagombea ambapo aliwataka wasipige makofi wala kushangilia wakati wagombea hao wakijinadi.
Kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha, Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya CCM katika nafasi ya ubunge ametangaza kuelekeza nguvu zake kwa vijana wasio na ajira kwa kuwawezesha kujiajiri na kujipatia kipato
Aliyasema hayo leo wakatia akizungumza katika kampeni ya kuwanadi wagomea Ubunge wa Chama cha mapinduzi CCM, mkoani Arusha katika kata mpya Sinoni , uliohudhuriwa na wagombwa 12 wa nafasi ya Ubunge
Nyari alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili Taifa kwa sasa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana na kuahidi kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini atahakikisha vijana wanajiajiri wenyewe
Alisema kuwa katika kusaidia hilo vijana watapewa elimu ya ujasiriamali na baaade kujiajiri wenyewe hali itakayosaidia kukua kwa uchumi wa Taifa letu na vijana kuongeza kipato chao
Akawataka vijana kuacha kutumika kuleta vurugu na badala yake wawe wamoja katika kuhakikisha wanaweza kujiletea maendeleo na si vingine kwani wao wamekuwa wakitumika katika sehemu mbali mbali bila kupata manufaa stahiki
“Nawaomba vijana mujiandae kwa ajili ya kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwani nimejipanga kuhakikisha mnapata elimu ya ujasiriamali ilimuweze kujiletea maendeleo na kuongeza kipato chenu na pato la taifa”alisema Nyari.
Kwa upande wake Mustapher Panju anaeomba kupewa tiketi na CCM ya nafasi ya ubunge aliwataka wagombea wenza katika kinyang’anyiro cha ubunge kupitia ccm kudumisha upendo,mshikamano,na umoja miongoni mwao vitakavyosaidia kukuza amani ndani ya chama na kuondosha makundi ambayo yamekuwa yakikiangusha chama katika chaguzi zilizopita.
Alisema kuwa changamoto za jimbo la Arusha anazijiwa hivyo wakimpa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM atahakikisha umoja,mshikamano na upendo vinatawala ili wananchi waweze kujiletea maendeleo.
Panju alisema kuwa atakapopitishwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya ubunge atahakikisha kuwa anal eta maendeleo tarajiwa kwa wakati kwani yeye atakuwa mtumishi wa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.
Naye Emmanuel Ole Njoro ameomba kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ya Ubunge ambapo alisea akipewa ridhaa atahakikisha kuwa anadumisha Amani mshikamano na umoja miongoni mwa jamii huku akiandaa mipango ya kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujifunza ujasiriamali ili waweze kujiletea maendeleo.
Alisema kuwa jografia ya jimbo la Arusha anaifahamu pamoja na changamoto zake hivyo anaowaomba wanachama wa CCM kuhakikisha wanampatia nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho
Kwa upande wake Thomas Munisi alisema kuwa tahakikisha changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo la Arusha anazipatia ufumbuzi pindi wanachama wa CCM watakapompatia ridhaa August 1
Alisema kuwa fedha za miradizinazokusanywa na halmashauri hazitachakachuliwa na zinaelekezwa katika miradi husika ilikuweza kulibadili jimbo la Arusha kwani nia na uwezo wa kuwatumikia wakazi wa jiji la Arusha anao hivyo ni wajibu kwa wagombea kuhakikisha wanakuwa wamoja,na mshikamano miongoni mwao.Chanzo http://mjengwablog.com

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...