Baada ya Emmanuel Okwi kutimka zake kwenda
Denmark, kocha wa Simba Dylan Kerr, ameamua kufanya jambo la maana mapema kwa
kugawa jukumu alililokuwa akilifanya Mganda huyo kwa mzawa Ibrahim Ajibu.
Ajibu amepewa mikoba ya Okwi ya kupiga mipira ya faulo baada ya kuonesha umahiri mkubwa wa upigaji adhabu hiyo mbele ya kikosi maalumu cha upigaji faulo kilichochaguliwa na Kerr.
Mbali na Ajibu, wachezaji wengine ambao wanashiriki zoezi hilo la upigaji faulo kwenye kambi inayoendelea visiwani Zanzibar ni Mussa Hassan ‘Mgosi’, Said Ndemla, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Hamis Kiiza.
Kocha Kerr alisema: “Ninaangalia ni wachezaji wapi wenye umakini wa kupima, pia wenye uwezo wa kupiga kwa nguvu na kwa maarifa.
“Hao watano ndiyo nilioanza nao, nitaendelea kuangalia wengine kwani kila mmoja anaweza kufanya kazi hiyo.”
Kocha huyo aliongeza kusema anavutiwa na Ajibu kwa uwezo wake wa kuyadanganya macho ya kipa pindi anapokuwa anapiga mpira.
Naye Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, alisema hao ni baadhi ya wachezaji walioonekana kuwa na ujanja na uwezo wa kupiga mipira ya faulo hasa ile inayotokea karibu na eneo la lango na kudai anaamini wanaweza kuwa warithi wa Okwi aliyetamba kwa mipira hiyo.
Katika zoezi hilo ambalo Kerr alitengeneza ukuta wa walinzi wanne na kipa mmoja golini, Ajibu alionekana kung’ara sambamba na Tshabalala ambaye alikuwa akipiga faulo hizo kwa umbali wa kama mita 20.

Comments