Fifa itafanya mkutano wake wa kongresi kumchagua rais mpya Februari 26, 2015.
Sepp Blatter alichaguliwa tena kama rais Mei 29 lakini siku nne
baadae alitangaza nia ya kujiengua kufuatia uchunguzi wa rushwa kwenye
shirikisho hilo la soka duniani.
Mgombea wa upinzani anapaswa kutajwa kabla ya Oktoba 26.
Rais wa Uefa Michel Platini ameombwa na wakuu wengi wa shirikisho hilo kuwania nafasi hiyo.
Comments