Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji
Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN
mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika Uwanja wa Nakivubo.
Stars ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza
soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza
wenyeji Uganda.
Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0
– 0 Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi
mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju
wa penati kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani
ya eneo la hatari.
Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo
langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82,
kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 – 1 Tanzania. Kwa
matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1
na sasa watakutana na Sudan.
Mara baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa
amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo
ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi
moja iliyopatikana.
Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu
kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko
yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa
muda mrefu ili kujenga timu bora.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya Jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir
Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said
Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan
Singano.
The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan
Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki
Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.
Comments