Wanasiasa
wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha Mgombea urais wa CCM, Dk John
Magufuli kutumia ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za
kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za
Taifa. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alisema walifuata taratibu zote kuikodi ndege hiyo na kwamba chama chake
ni kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo.
Source: Mwananchi
Source: Mwananchi

Comments