50 Cent alipata umaarufu mkubwa baada ya kuzindua albamu yake ya “Get Rich or Die Trying” katika mwaka wa 2003.
50 Cent mwenye umri wa miaka 40 aliwahi kuuza albamu milioni 30 na pia aliwahi kushinda tuzo ya Grammy.
50 Cent alipata mafanikio makubwa katika biashara kama ilivyokuwa
katika muziki huku akipiga hatua kubwa alipouza kampuni yake ya maji VitaminWater kwa Coca-Cola katika mwaka wa 2007.
50 Cents amejisajili kupata hifadhi kupitia kifungo cha 11 ambacho kitamkinga dhidi ya mashirika na watu wanaomdai hadi atakapoweza kurekebisha hali yake ya kifedha.
Wakili wa 50 Cent William A Brewer alisema kuwa biashara ya mwanamuziki huyo bado zitaendelea
Comments