Omar Sharif muigizaji wa Misri ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake katika filamu za "Lawrence of Arabia" na "Doctor Zhivago" aliaga dunia mnamo Ijumaa akiwa na umri wa miaka 83.
Omar Sharif alikuwa akipokea matibabu kutoka hospitali moja mjini Cairo baada ya kupatikana na ugonjwa wa Alzeima.
Omar Sharif alitwaa tuzo mbili za Golden Globe na pia kuteuliwa kuwania tuzo za Oscar kutokana na mchango wake katika filamu mashuhuri ya Lawrence of Arabia ya mwaka wa 1962.
Katika mwaka wa 2003 Omar Sharif pia aliigiza katika filamu ya Kifaransa ya Monsieur Ibrahim ambapo aliigiza kama mwenye duka wa asili ya Kituruki aliyejaribu kufanya usuhuba na kijana myahudi.
Comments