AZAM TV KUONYESHA PREMIER LEAGUE KWA KISWAHILI
Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga
nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.
Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha
unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa
kuanza mapema mwezi ujao.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.
“Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika
ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo,
tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.
“Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu
ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika
ubora wa hali ya juu zaidi,” alisema Tido.
Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao
matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.
Comments