Shangwe za shujaa; Farid Malik Mussa akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Azam FC leo dhidi ya KCCA Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM CHIPUKIZI aliyepandishwa kutoka akademi mwaka juzi, Farid Malik Mussa leo amekuwa shujaa wa Azam FC baada ya kufunga bao pekee lililoiwezesha timu hiyo kutinga Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Farid mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao hilo dakika ya 76 kwa ustadi wa hali ya juu, baada ya kuruka juu kwenda kuunganisha kwa guu la kushoto krosi ya Ame Ally ‘Zungu’. Azam FC sasa itamenyana na Gor Mahia ya Kenya katika fainali Jumapili- hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufika hatua hiyo, baada ya awali, mwaka 2012 kufungwa na Yanga SC 2-0 Dar es Salaam pia. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Suleiman Ahmed wa Djibouti aliyesaidiwa na Yatayew Balachew wa Ethiopia na Nagi Ahmed wa Sudan, kipindi cha kwanza timu zo...