Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe leo.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.
Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari.
Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.(P.T)
MBUNGE wa
Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana
huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini
Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama
hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa
amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa
uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba
endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama,
malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani
“Hivyo, kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.
“Hivyo, kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.
Lissu
aliongeza kuwa hata kama Zitto angeweza kwenda kushitaki lazima
angeanzia katika mahakama ndogo za wilaya yaani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi au Masijala ya Mahakama ya Wilaya tofauti na alivyopeleka
kesi hiyo moja kwa moja Mahakama Kuu.
Mahakama
hiyo pia imemtaka mbunge huyo wa zamani kukilipa chama hicho gharama
zote za kesi hiyo kama ilivyoelekezwa na mahakama, na kwa mujibu wa
Lissu, Chadema kitakaa na kutathmini gharama husika.
Kuhusu utambulisho wa Zitto bungeni, Lissu alisema kwa mujibu wa kanuni za chama chake, katibu wa chama chake anatakiwa kumwandikia barua Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kumjulisha Zitto tena si mwanachama wao na taratibu zingine zitafuatia.

(PICHA/HABARI NA DENIS MTIMA/GPL)
Comments