LONDON, England
BAADA ya mashabiki wa Manchester United kuwazomea wachezaji wa timu hiyo katika mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi paka weusi Sunderland, Kocha Louis Van Gaal amekuja juu na kuwataka wachezaji wake kutorudisha mpira mara kwa mara kwa kipa David de gea.
Mashabiki hao waliokuwepo katika mechi hiyo iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford, waliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuonekana kukasirishwa na kuchoshwa na wachezaji wao kutofanya mashambulizi na kurudisha mipira mara kwa mara kwa kipa wa timu hiyo.
"Ninakubaliana na mashabiki, hatutakiwi kumtumia kipa mara kwa mara. Kuna muda tunapata nafasi ya kushambulia lakini hatufanyi hivyo, tunamchosha De gea " alisema Van Gaal.
Kocha huyo raia wa uholanzi,jana alikuwa na kibarua kizito kukiongoza kikosi chake kiliposhuka katika uwanja wa St.James Park kuwavaa Newcastle United ambao wamekuwa katika kiwango kizuri kwa mechi za hivi karibuni.
Comments