Skip to main content

MASTAA NA SIASA


Chande abdallah
ILIKUWA kama kitu cha ajabu baada ya mastaa wa fani mbalimbali nchini hasa wa muziki na filamu, kutangaza nia zao za kujiingiza kwenye masuala ya siasa ambapo mpaka sasa mastaa kama Profesa Jay na Afande Sele wameweka wazi nia zao huku mastaa kama Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini na Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakiwa ni baadhi ya mastaa waliotinga bungeni tangu uchaguzi uliopita.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu'.
Bongo siyo nchi pekee ambayo suala hilo limejitokeza, bali hata kwenye nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani limewahi kutokea ambapo kwa nyakati tofauti mastaa wakubwa wamewahi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali huku wengine wakishindwa na wengine kushinda nafasi za kuwakilisha wananchi katika nyadhifa mbalimbali. Wafuatao ni baadhi ya mastaa wakubwa wa majuu ambao wamewahi au wanaendelea kushiriki kwenye siasa:-

SCHWARZENNEGGER.
ARNOLD SCHWARZENNEGGER
Huyu ni staa mkubwa wa filamu za 'action' nchini Marekani ambaye anajulikana sana kwa umbo lake kubwa. Jamaa alianza kama mtunisha misuli na kuingia kwenye tasnia ya filamu ambapo alifanya vema na muvi zake kama Terminator na Predator. Arnold alianza siasa mwaka 2003 ambapo aligombea ugavana wa Jimbo la Calfornia na kushinda, alishikilia nafasi hiyo hadi mwaka 2011.
SCHWARZENNEGGER.
ARNOLD SCHWARZENNEGGER
Huyu ni staa mkubwa wa filamu za 'action' nchini Marekani ambaye anajulikana sana kwa umbo lake kubwa. Jamaa alianza kama mtunisha misuli na kuingia kwenye tasnia ya filamu ambapo alifanya vema na muvi zake kama Terminator na Predator. Arnold alianza siasa mwaka 2003 ambapo aligombea ugavana wa Jimbo la Calfornia na kushinda, alishikilia nafasi hiyo hadi mwaka 2011.
ANDRIY CHEVSHENKO.
ANDRIY CHEVSHENKO
Ni msakata kabumbu raia wa Ukraine ambaye alipata mafanikio makubwa katika historia ya soka duniani ambapo alichezea klabu kubwa duniani kama AC Milan na Chelsea. Alitangaza kustaafu mwaka 2012 baada ya kucheza soka kwa muda mrefu. Baada ya kustaafu alijiunga na Chama Cha Demokrasia cha Ukraine akigombea nafasi ya ubunge, hata hivyo alishindwa kupata nafasi hiyo kutokana na ushindani mkubwa uliojitokeza.
WYCLEF JEAN
WYCLEF JEAN
Ni staa wa muziki toka Marekani aliyehamia nchini humo akiwa na familia yake kama wakimbizi waliotokea nchini Haiti. Jamaa aliwika na ngoma zake kama 911, Two Wrongs na Hips Don't Lie aliyoshirikiana na Shakira. Jamaa alijitosa kwenye siasa mwaka 2010 akitangaza kugombea nafasi ya urais katika nchi yake ya kuzaliwa ya Haiti ambapo hata hivyo alitolewa kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na sababu za makazi yaani kuishi Marekani zaidi kuliko Haiti.
YOUSSOU N'DOUR.
YOUSSOU N'DOUR
Huyu ni staa mkubwa zaidi Afrika ambaye anatajwa kushika namba moja kwenye orodha ya wasanii wa muziki matajiri Afrika huku Jarida la Rollingstone likimtaja kama mwanamuziki anayejulikana sana Afrika.
Mwanamuziki huyu anayejulikana Afrika na duniani kwa kibao chake cha Dirima, alitangaza nia ya kugombea urais mwaka 2012 lakini akatolewa kwenye kinyang'anyiro hicho kutokana na saini za wadhamini wake kuwa na kasoro na pia kutokana na ushawishi wake aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni ambapo anaendelea na nafasi hiyo hadi hivi sasa.
MANNY PACQUIAO.

Jina lake kamili ni Emmanuel Dapridran Pacquiao ni mkali wa ndondi tokea Ufilipino mwenye heshima na mafanikio makubwa duniani kwa ujumla. Pamoja na mafanikio yake alitangaza kujiingiza kwenye siasa mwaka 2007 lakini alishindwa kiti cha baraza la uwakilishi katika Jimbo la Manila na mwaka 2009 aliamua kugombea tena kupitia Jimbo la Sarangani ambapo alishinda kwa kishindo kikubwa bila pingamizi chochote ambapo pamoja na masuala ya ngumi anaendelea kushika nafasi hiyo hadi hivi sasa.CHANZO:GLOBALPUBLISHERS

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...