Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Nachingwea kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe 18.3.2015.
Mamia ya wanavikundi na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika Mkoa wa Lindi zilizofanyika Nachingwea wakifuatilia kwa makini sherehe hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha waalikwa zawadi mbalimbali alizopewa na wanavikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe mkoani Lindi. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu Nachingwea tarehe 18.3.2015
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya
wananchi na wana vikundi vya WAMA katika Mradi wa Mwanamke Mwezeshe
katika sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi hivyo zilizofanyika
Nachingwea tarehe 18.3.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete, akimkabidhi cheti kwa Bi Fatuma Mchia,
Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya WAMA Kwenye Mradi wa Mwanamke
Mwezeshe kwa kuvuka lengo kwa kuingiza wanavikundi wengi kwenye mradi
huo.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma
Kikwete akianzisha mchango wa papo kwa papo kwa ajili ya Mradi wa
Mwanamke Mwezeshe na kufanikiwsa kukusanya zaidi ya shilingi milioni
moja.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachuo wanaosomea ualimu kwenye
Chuo cha Ualimu Nachingwea mara baada ya kuhudhuria sherehe za kutimiza
mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe
zilizofanyia chuoni hapo tarehe 18.3.2015.
Mke wa
Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma
Kikwete akishiriki katika mkutano wa ndani wa Chama cha Mapinduzi
wilayani Ruangwa akitokes Nachingwea ambako alihudhuria sherehe za
kutimiza mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe
tarehe b18.3.2015.
Mke wa
Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM,Mama Salma Kikwete akiwasalimia
wananchi wa Kijiji cha Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa ambao
walijikusanya kwa wingi hadi kupelekea Mama Salma kusimama na kuzungumza
nao. Mama Salma Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku
tano.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya
Mnacho iliyoko wilayani Ruangwa. Mama Salma alikwenda shuleni hapo
kukabidhi madawati 100 aliyowaahidi wakati alipozuru shule hiyo mwaka
jana.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya
Mnacho iliyoko wilayani Ruangwa. Mama Salma alikwenda shuleni hapo
kukabidhi madawati 100 aliyowaahidi wakati alipozuru shule hiyo mwaka
jana.
Comments