Ripoti kutoka Nigeria zinadai
kuwa kundi la kigaidi la Boko Haram limewateka nyara watu zaidi ya 400
katika mji wa Damasak ulioko kaskazini mwa nchi hiyo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, Boko Haram liliwateka
nyara watu hao na kuondoka nao wakati mji huo ulipokuwa ukikombolewa na
vikosi vya Niger na Chad.
Watu zaidi ya 400 hawajulikani waliko wengi wao
wakiwa wanawake na watoto na inasemekana kuwa, Boko Haram imeondoka na
raia hao wakati walipolazimika kuukimbia mji huo.
Baadhi ya duru kutoka Damasak zinaripoti kwamba,
zaidi ya watoto mia nne wenye umri wa takribani miaka 11 nao wametekwa
nyara na Boko Haram.
Serikali ya Nigeria imechukua hatua kali za usalama kabla ya uchaguzi wa Rais na Bunge ulizopangwa kufanyika Jumamosi ijayo.
Comments