Nyota wa Sampdoria Samuel Eto’o akipokea tuzo hiyo kutoka kwa rais wa ECTR Moshe Kantor mjini London
Nyota wa soka Samuel Eto’o alitunukiwa siku ya Jumatatu kwa msimamo
wake wa hamasa dhidi ya ubaguzi wa rangi, huku waandaaji wa tuzo hiyo
wakionya kuwa tabia hizo bado zipo kwenye soka barani Ulaya.
Mshambuliaji wa zamani wa Cameroon na Barcelona alipokea medali ya
Medal of Tolerance kutoa Baraza la Ulaya la Uvumilivu na Mapatano kwenye
hafla ya chakula cha jioni kwenye hekalu la London Kensington.
Eto’o akionyesha tuzo yake
Eto’o ambaye anaichezea Sampdoria ya Italia, anakumbukwa kwa kutoka
uwanjani wakati wa mechi ya Hispania mwaka 2006 baada ya kufanyiwa
ubaguzi.
“Tangu siku hiyo, niliamua nitasimama na kupambana dhidi ya
unyanyasaji huu,” alisema baada ya kupokea tuzo yake, huku akisindikizwa
na Eden Hazard wa Chelsea, Kolo Toure wa Liverpool na kiungo wa zamani
wa Barcelona Deco.
“Njia pekee ni kusimama na kukemea.”
Comments