Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C,
Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani
wakiingia watazamaji 36,693.
Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu
mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi
sh.11,669,600.
Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29,
Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh.
11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 huku Yanga wakipata
sh.81,727.83.
Wakati huo huo Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho siku ya jumanne
katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro
watawakaribisha Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.
Comments