Mkuu wa
mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha
viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa
mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin
Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi
na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza
katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara
kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa
mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
Mratibu
wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye
migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani
Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia
katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya
mipaka inasababishwa na wanasiasa.
Baadhi ya
watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa
wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti
Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza
na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.
Wananchi
wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo
pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi
inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri
ya wilaya ya Babati.
Wananchi
wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi
ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao
kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa
sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na
wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu
migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa
Manyara.
Baadhi ya
watendaji wa wizara ya ardhi wakiratibu malalamiko ya wananchi katika
kikao kilichofanyika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Babati,mkoa wa
Manyara.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya
migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza
kero za ardhi. Source Mjengwa.
Comments