Julius Mtatiro
--
NITAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA – DAR ES SALAAM.
Ndugu zangu, kesho Jumatatu 09 Machi 2015 saa 4.00 asubuhi, nitachukua
fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Segerea kama ambavyo taratibu za
ndani ya chama changu zinaruhusu. Hakutakuwa na mbwembwe vifijo wala
nderemo kwa sababu bado hatutajajua kwa hapa Dar Es Salaam jimbo gani
litaachwa kwa chama gani au ikiwa wagombea wa vyama vyote vya UKAWA
watakutanishwa na kupigiwa kura ya maoni, vyovyote vile iwavyo niko
tayari kukabiliana na demokrasia ya ndani ya chama changu na hata ndani
ya UKAWA.
Hivi sasa nina umri wa miaka 32 tu lakini nikiwa
nimepitia kila aina ya uzoefu wa kiuongozi, kisiasa n.k. Naamini kuwa
nina uzoefu wa kutosha kuwavusha wana Segerea mahali ambako nimeishi kwa
takribani miaka 12 huku shughuli zangu zote za ujasiriamali zikiwa
jimboni humu. Ninalifahamu jimbo hili vizuri, watu wake, matatizo yao na
changamoto zinazowakabili. Zaidi ya yote nina uwezo wa kushirikiana na
wananchi tukioneshana njia ya kuzitatua changamoto hizi na wakati
ukifika nitazieleza huku nikiweka wazi njia za kupita.
Pamoja na
kwamba nina elimu ya darasani ya kutosha, uzoefu wa uongozi usio na
shaka na tabia na mienendo ya maadili huku nikiwapenda watu wa kila
namna, natambua kuwa kazi ya kuwa mbunge ni zaidi ya hayo, inahitaji
weledi, wepesi, staha na heshima, kujali, kuwa karibu na watu na
kujitolea kwa hali na mali kuwapigania wale ambao haki zao na mahitaji
yao yanacheleweshwa – kaliba ya namna hii imejengeka na sina shaka kuwa
ninakidhi sifa na vigezo hivi vya nyongeza.
Mimi ni muumini wa
demokrasia, nitasaidia wagombea wote waliojitokeza kunipinga na
kushindana nami ikiwa kutakuwa na haja hiyo, sitamtukana wala kumsema
vibaya yeyote yule, kazi yangu kuelekea Oktoba ni kujinadi na kueleza
sifa zangu na uwezo wangu huku nikivihusianisha na utatuzi wa matatizo
ya wananchi wa Segerea kwa kushirikiana na wananchi.
Nawaomba
wanachama wengine wa vyama vya UKAWA wenye sifa, vigezo na uwezo
wajitokeze kwa wingi. Sote tutapimwa kwa uwezo na vigezo vyetu na mwisho
wa siku atapatikana mmoja wetu na ataungwa mkono na sisi sote. Baada ya
Oktoba 2015, Segerea itakuwa na mpambanaji mpya, mbunge wa wananchi na
atakayepigana hadi tone la mwisho la damu kwa ajili ya wananchi wake. Na
labda mtu huyo atakuwa ni mimi.
Nawatakia kila la heri na kwa ambao wangependa kunifahamu zaidi wanaweza kusoma katika kiunganishi hiki www.facebook.com/ JuliusSundayMtatiro/posts/ 578218822317742:0
Julius Mtatiro, +255 787 536 759, 0755 855 144, Juliusmtatiro@yahoo.com
Julius Mtatiro,
Cert in Linguistics(Nairobi), B.A(Hons)- Dar, M.A(Hons)- Dar, LLB (Candidate) - Dar,
Freelance Translator and Private Consultant in
Administration, Education and Political Science.
P.O Box 10979,
Dar Es Salaam,
Phone; +255717536759+255787536759,
Email; juliusmtatiro@yahoo.com.
Cert in Linguistics(Nairobi), B.A(Hons)- Dar, M.A(Hons)- Dar, LLB (Candidate) - Dar,
Freelance Translator and Private Consultant in
Administration, Education and Political Science.
P.O Box 10979,
Dar Es Salaam,
Phone; +255717536759+255787536759,
Email; juliusmtatiro@yahoo.com.
Comments