Ni mwaka wenye hadhi na uzito kwa
mcheza tennis Andy Murray, hali hiyo si tu kutokana na matumaini yake ya
kuongeza taji la pili la Grand Slam bali ni mpango alionao wa kufunga
ndoa na mpenzi wake Kim Sears April mwaka huu.
Mchezaji huyo raia
wa Scotland amerejea katika nafasi ya nne duniani baada ya awali
kuporomoka kutokana na upasuaji wa mgongo aliofanyiwa.
Furaha ya
mchezaji huyo inachagizwa zaidi kutokana na rekodi mpya aliyojiwekea
baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali katika mashindano ya Indian
Wells yanayoendelea huko California Marekani.
Comments