Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Simon Sserunkuma, amesema kuwa
kwasasa hana furaha ndani ya klabu ya simba kutokana na kukosa nafasi
ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Goran Kopunovic.
Nyota huyo alisajiliwa wakati wa msimu wa dirisha dogo msimu akitokea
kwenye klabu ya Express ya Uganda, kipindi hiki amekuwa na wakati mgumu
kutokana na kuwekwa katika risiti ya wachezaji wa akiba kwenye michezo
mingi.
Akizungumza na mwandishi wetu mchezaji huyo amesema kwasasa anatamani
kuondoka klabuni hapo ili akatafute sehemu ambapo ataendelea kuimarisha
kiwango chake.
Comments