Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA, Tundu Lissu
leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kasikani Zitto
Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia
mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
“Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote
anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa
katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza
rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema.
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa mahakamani
leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya Jaji Mpya,
pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa statement.
Licha ya kutupilia mbali kesi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe, Mahakama kuu imemtaka kulipa gharama zote za kesi toka
ilivyoanza.
Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kikao cha
Kamati Kuu kumjadili na hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu
kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Chanzo: EATV
Comments