Ivory Coast kujiunga na Chad, Cameroon na Niger katika vita dhidi ya Boko Haram.
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema kuwa Ivory Coast itajiunga na nchi zingine za Afrika Magharibi katika kukabiliana na kundi la kigaidi la Boko Haram.
Rais Ouattara
alisema hivyo katika kongamano la mabalozi mjini Abidjan ambapo aliahidi
kutuma kikosi cha majeshi kujumuika na vikosi vya Cameroon, Chad na Niger katika kukabiliana na kundi hilo la kigaidi.
Pia Ivory Coast itafanya mkutano na nchi wanachama wa ECOWAS ili kupanga mkakati wa kukabiliana na Boko Haram.
Comments