Mjengo huo wa Diamond uliopo maeneo ya Madale nje kidogo ya Jiji la Dar, unadaiwa kufikisha thamani hiyo kutokana na kuwa na vyumba vinne vya kulala, bwawa maalum la kuogelea (swimming pool), sehemu ya mazoezi (Gym), jakuzi, kaunta ya vinywaji, ukumbi wa kuchezea, studio ya muziki, uwanja wa mpira wa kikapu na sehemu ya kuchezea mchezo wa mishale (Darts)
Kwa mujibu wa Diamond, nakshi za dhahabu alizoziweka katika kuta za bafu na chooni pekee, zimemgharimu sh. mil. 70 kitu kinachoendana na utabiri wa mkandarasi huyo kuwa nyumba hiyo inafikia thamani ya zaidi ya sh. mil. 400.
Jikoni.
Akiuzungumzia mjengo huo baada ya
kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini,
alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani umechukua
nafasi kubwa, na 'material' yaliyojengea ni ya gharama.
"Ukitazama kwa makini, material nyingi
zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za
kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea," alisema mkandarasi
huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za
mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila
kupokelewa.
Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa
haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema
imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo
wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi
namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na
mvua zinazoendelea kunyesha. CHANZO: GLOBAL PUBLISHER
Comments