LAS VEGERS, Marekani
MWANAMUZIKI ambaye ni rapa mahiri nchini Marekani 50 Cent, ametabiri kwamba bondia Floyd Mayweather Junior, atampiga mpinzani wake Manny Pacquao katika pambano litakalofanyika Mei 2, mwaka huu.
50 Cent katika utabiri wake huo amesema ataweka dola milioni 1.6 za Marekani na kama kweli Mayweather atashinda kwenye pambano hilo litakalopiganwa Las Vegers, atapata dola milioni 2.3.
Akihojiwa katika kipindi cha Breakfast Club 50 Cent alisema; "Nimepata bingwa, bingwa atampiga mpinzani na kushinda na kuonekana kwamba hakukuwa na sababu ya kupigana."
Mkali huyo wa kurap alisema alikwenda kumfuata Mayweather katika onesho la Cris Brown kwenye Ukumbi wa Baclays Centre, New York kwa ajili ya hicho anachokisema.
Wakali hao wa ndondi duniani tayari wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo ambao unatajwa kuwa ghali zaidi duniani.
Comments