Mwakilishi wa katibu mkuu katika nchi za Afrika Magharibi Mohamed ibn chambas
Mapambano yanayoendelea dhidi ya magaidi wa boko haramu kaskazini mwa
nchi ya Nigeria yanaonekana kuungwa mkono na mashirika mawili ya
kimataifa.
Msemaji wa jeshi la anga la Nigeria alithibitisha kupokea taaarifa
hiyo kutoka kwa mwakilishi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa katika
nchini za magharibi mwa Afrika, Mohamed ibn chambas.
Mwakilishi huyo amesema kuwa”ni muda wetu sote kupambana na kusitisha
shughuli za Boko Haram katika ukanda wetu na kuunganisha nguvu ya
pamoja kupambana na kikundi hiki, mapigano dhidi ya Boko Haramu yamekuwa
ya kimataifa na Afrika nzima na ninaamini majeshi ya Chad yatatuunga
mkono kwenye mapambano haya”.
Chambas ameongeza kwamba “kipaumbele cha umoja wa mataifa ni
kuimarisha mapambano dhidi ya magaidi wa boko haramu ambao wamesababisha
matatizo makubwa nchini Nigeria pia katika nchi jirani za Kameruni,
Niger na Chad”.
Comments