Dr Evarito Mtitu
Na MatukiodaimaBlog
MVUTANO
mkali ubunge jimbo la Kalenga baada ya mpinzani wa
Jackson Kiswaga kutoka kata ya Nzihi Msomi Dr Evaristo
Mtitu kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la
Kalenga linaloongozwa na Godfrey Mgimwa (CCM)
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz Dr.
Evaristo Andreas Mtitu alisema kuwa amelazimika kujitokeza kuwania
ubunge katika uchaguzi mkuu mwaka huu kupitia chama cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema)
Dr Mtitu
alisema kuwa yeye ni mzaliwa Kidamali kata ya Nzihi
katika halmashauri ya wilaya ya Iringa
alizaliwa mwaka (1974) na kusoma Shule ya msingi Nyamihuu olevel
Ulayasi secondary 1995. Alevel Mzumbe high school morogoro 1998,
Pia baada
ya hapo alijiunga na Stashahada ya ualimu Chuo cha ualimu Morogoro
2001. Shahada ya kwanza ya Elimu, Chuo kikuu DSM, 2006. Shahada ya
uzamili katika elimu, Chuo Kikuu cha Charles Darwin, Australia, 2009.
Dr
Mtitu pia alisema amehitimu Shahada ya uzamivu (Doctor of Philosophy)
katika elimu Chuo Kikuu cha VICTORIA cha Wellington, New Zealand,
2014.
Akielezea kazi
ambazo amepata kufanya katika nchi kuwa ni pamoja na ualimu Shule
za sekondari , mkufunzi vyuo vya ualimu Tandala na Klerruu huku
kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania aliyebobea
katika taaluma ya mitaala ya elimu na ufundishaji,
Katika Nyanja ya utandawazi
alisema yeye ni mtafiti, elimu ya geography, sera mipango na uongozi
katika elimu na nadharia ya upembuzi.
Hivyo alisema kuwa lengo lake
la kutaka ubunge jimbo la kalenga ni kushirikiana na wana
Kalenga katika kuleta maendeleo .
Kipaumbele chake
ni kuboresha elimu na huduma za afya ,miundo mbinu huku
akimpongeza mbunge wa sasa Bw Mgimwa kuwa
amejitahidi kufanya kazi kulingana na uwezo wake kwa muda mfupi
ila bado kuna haja ya kumuunga mkono kwa kumsaidia zaidi
kwa kuliunganisha jimbo hilo na wahisani wa ndani na nje.
Kujitokeza
kwa Dr Mtitu katika kata hiyo ya Nzihi kutafanya kata moja
hiyo kuwa na wagombea wagombea watatu hadi sasa wanaotaka ubunge
kutoka kata hiyo .
Comments