Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, akiwa na mume wake, Emmanuel Mbasha.
KESI ya
kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba
Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama
ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa
siri.
Kesi hiyo
ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5
hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya
Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa
ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali,
Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.
Siku
hiyo, shahidi namba nne ambaye ni daktari anatarajiwa kutoa ushahidi
wake na mshitakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana. Mbasha anashtakiwa
kwa makosa mawili ya ubakaji, la kwanza anadaiwa kulifanya Mei 23, mwaka
jana, eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na
Mei 25, mwaka jana akidaiwa kutenda kosa hilo kwa binti huyo kwa mara
nyingine eneo hilohilo.
(HABARI:HARUNI SANCHAWA/GPL)
Comments