Zaidi ya Sh. Bilioni 56 za Tanzania zimetumika kutengeneza studio
mpya za kisasa za Azam TV, zilizopo eneo la Tabata Relini jijini Dar es
Salaam.
Hayo yamesemwa na Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido
Mhando wakati akizungumza leo mchana katika Mkutano na Waandishi wa
Habari Tabata Dar es Salaam.
Tido Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza kampuni kubwa za vyombo vya
habari zikiwemo Idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) na Mwananchi Communication Limited (MCL) amesema studio hizo zina
ubora kuliko nyingine zote nchini.
“Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na studio za kampuni
kubwa kama CNN, Al Jazeera, BBC na zinaweza kuwa na ubora kuliko studio
zote za hapa nchini,”amesema Tido.
Tido amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa studio hizo zoezi la uzinduzi wake rasmi litafanyika kesho asubuhi.
Mhando amesema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Comments