Kiongozi wa kidikteta wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amejaribu
kuonesha namna anavyojali masuala ya kijinsia kwa kuwapelekea askari wa
kike poda za kujipodolea
katika kambia ya kijeshi ya ndege za mashambulizi ya anga
aliyoitembelea wakati dunia ikiadhimisha kilele cha siku ya wanawake
duniani.
Kiongozi huyo wa kipekee asiyetabirika alituma salamu zake za pongezi
kwa wake wa askari wa kikosi cha anga katika sherehe za wanawake
ulimwenguni na kusherehekea mafanikio na mchango wa wanawake popote,
wakati alipokitembelea kikosi cha siri cha anga na kukagua nguvu za
kituo hicho kipya.
Kwa mujibu wa taarifa za ziara yake, kiongozi huyo hakukutana ana kwa
ana na mwanamke yeyote lakini aliwataka maafisa wake kukabidhi zawadi
alichowapelekea askari wake ikiwemo vipodozi alivyowapelekea wanawake
walioko katika jeshi hilo kama zawadi.
Kiongozi mkuu Kim alijieleza kama balozi wa nishati ya kijanai na
kueleza nia ya kutumia nguvu ya upepo,sola na hata nishati kwa ujumla
ili kukwamua tatizo la umeme nchini mwake ambako umeme umekuwa ukikatika
katika kila uchao.
Wakati akifanya ukaguzi huo katika ziara hiyo hakusita kumsifu baba
yake Kim Jong-ill,kwa kumwelezea kuwa alikuwa mwenye
Imani,mzalendo,aliyepambana na ubeberu wa kielimu na maadili ya kielimu.
Kim yeye mwenyewe alisoma mjini Geneva inaaminika kuwa ana miaka 32,
alipiga picha ya pamoja na marubani wake ,huku akiwataka wawe tayari
wakati wowote na kuwakumbusha kauli mbiu yao ya kusubiri amri ya chama
ili kutekeleza mipango yao.
Ziara hiyo pia imechukuliwa kama ziara ya mafunzo,huku vifaa mbali
mbali vikigawiwa kama vyoo,vifaa vya kulia,vifaa vya jikoni,mahema ya
uzalishaji mazao na zana za chumba cha kuzalishia uyoga.
Msafara wake ulielekea katika kituo hicho kwa kutumia ndege yake binafsi ya Soviet-era IIyushin Il-62.
Comments