Kocha Mkuu wa timu ya Daraja la Kwanza ya Friends Rangers yenye
maskani yake Magomeni Kagera, Dar es Salaam, Ally Yusuf’Tigana’amesema
kuwa wanajipanga vilivyo ili kuanza mazoezi ya pamoja mapema.
Tigana alisema hatua hiyo ina lengo la kujiandaa vyema, alisema kabla
ya kikosi hicho kushiriki kwenye michuano ya msimu ujao ya Ligi Daraja
la Kwanza(FDL).
Alisema anaamini kwa kufanya hivyo kutawasaidia wachezaji wake,
alisema kujiweka fiti kabla ya kuingia kwenye michuano hiyo ambayo
hatima yake huwa ni kupatikana kwa timu zitakazocheza Ligi Kuu Tanzania
Bara.
“Ni kweli kuwa mara tu baada ya kumalizika kwa ligi ya FDL, wachezaji wote wamepewa mapumziko.
“Lakini nitawasiliana haraka na viongozi ili kuangalia uwezekano wa kuanza mazoezi yetu mapema,”alisema Tigana.
Tigana alisema hivi sasa kila mchezaji anafanya mazoezi binafsi huko
waliko, alisema lengo likiwa ni kuendelea kujiweka vizuri bila ya kujali
kuwa ligi ya FDL imemalizika.
Kocha Tigana alisema anaamini msimu ujao atahakikisha wanafanya
maandalizi mazuri, alisema hiyo ikiwa ni pamoja na kusajili vizuri na
anaamini kwa kufanya hivyo kutatimiza ndoto zao za kucheza ligi kuu
Tanzania Bara.
Comments