TIMU inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini Prisons imekanusha uvumi wa taarifa zilizozagaa kwamba wako mbioni kumtimua Kocha Mkuu wa klabu hiyo David Mwamaja kufuatia matokeo mabovu ya klabu hiyo kwa msimu huu.
Jumamosi liyopita timu ya Tanzania Prisons ilikubali kipigo cha magoli 5-0 kutoka kwa Simba mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa na kushuhudia ‘wajelajela’ wakiendelea kukata tamaa ya kujinusuru na kushuka daraja msimu huu.
Katibu Mkuu wa klabu ya Tanzania Prisons Osward Morris, alisema habari hizo si za kweli na ni uvumi tu unatakiwa kupuuzwa, Prisons bado inaimani na Mwamaja na kwa sasa bado anaendelea kurekebisha makosa yaliyopo kwenye kikosi chake.
“Taarifa za kumfukuza Mwamaja si za kweli, hilo ni suala la uongozi na maamuzi hayachukuliwi pupa pupa. Sio suala la haraka, linahitaji muda na utaratibu,” alisema Morris.
Lakini pia akakanusha madai kwamba, kufanya vibaya kwa Prisons kwenye ligi msimu ni kwa sababu ya ukata.
“Hakuna kitu kama hicho, timu inapata mahitaji yote muhimu lakini kufanya vibaya kwa timu pia kunachangiwa na saikolojia ya wachezaji kutojiamini baada ya kupoteza michezo mingi kwenye msimu huu,” aliongeza Morris.

Comments