LONDON, England
LIGI kuu England, iliendelea usiku wa kuamkia jana kwa viwanja vitatu tofauti kuwaka moto.
Aston Villa walikuwa wenyeji wa West Brom, hadi mwisho wa mchezo wao, wenyeji wakaibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo umeiondoa, Aston Villa katika kundi la timu tatu za mwisho zitakazoteremka daraja.
Katika mchezo mwingine, Hull City walishindwa kutamba nyumbani walipomenyana na Sunderland na kulazimishwa sare ya bao 1-1, huku Southampton ikinyakua pointi tatu muhimu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Ligi hiyo iliendelea tena jana kwa Manchester City kuwakaribisha Leicester City, wakati Manchester United walikuwa ugenini kuvaana na Newcastle.
Arsenal walikuwa wageni wa QPR, huku Liverpool ikipepetana na Burnley. Katika viwanja vingine West Ham walikuwa wenyeji wa Chelsea, Totthenham wakicheza na Swansea, na Everton walisafiri kucheza dhidi ya Stoke City.
Comments